DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE

KSh550.00

Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi usio wa kawaida. Umeleta pamoja waandishi stadi wenye macho makali, na wanaolenga moja kwa moja kwenye kiini bila hofu yoyote. Waandishi wanaotambulika kwa haraka ni kama vile Muhammed Said Abdulla, Said A. Mohamed, Ken Walibora, Farouk Topan na wengineo. Mkusanyiko huu pia haukuacha waandishi shupavu wanaochipuka kama vile Doreen Baingana. Mohammed Khelef Ghassany na wengineo.Mkusanyiko huu umeshughulikia upana wa kimaudhui na mitindo mbalimbali ya uandishi. Isitoshe, waandishi wametumia vyema uhuru wa kisanii kwani hadithi mwanana ni kama ndoto ambayo haiwezi kulazimishwa kutii sheria hususa za ndivyo au sivyo. Kila hadithi katika mkusanyiko huu ni ya aina yake na itamsisimua, itamburudisha na kumfunza msomaji.Utangulizi wa kina umetolewa kuhusu hadithi fupi ili kuwaelewesha wasomaji jinsi utanzu huu ulivyo tofauti na tanzu nyingine za fasihi.

Quantity:

There are no reviews yet.

Add your review